10.5 C
New York

Huyu ndiye Michael Kuka; shabiki aliyegeuka kivutio AFCON 2025

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KAMA umefuatilia kwa karibu mechi zote za msimu huu wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), basi sura yake si ngeni machoni mwako.

Anaitwa Michel Kuka Mboladinga, shabiki kindakindaki wa timu ya taifa ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Staili yake yazua gumzo

Kuka amekwenda katika fainali hizo zinazofanyika Morocco akiwa na staili yake ya pekee iliyogeuka kivutio kwa mashabiki wa soka barani Afrika.

Katika mechi zote za DRC, kabla ya timu hiyo kuondoshwa na Algeria, Kuka amejizolea umaarufu kutokana na staili yake ya kusimamia mwanzo hadi mwisho wa mechi. Ni jumla ya dakika 438.

Kivutio zaidi ni namna alivyoweza kuganda kwa dakika 90 za kila mchezo, huku akiwa amenyayua mkono wake wa kulia, kama linavyoonekana sanamu la Waziri Mkuu wa kwanza wa DRC, Patrice Lumumba, lililoko mjini Kinshasa.

Historia inakumbusha kuwa Lumumba ndiye aliyeongoza harakati za uhuru wa DRC kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960 lakini aliuawa mwaka mmoja baadaye.

Kama ilivyo kwa sanamu, Kuka huvalia suti ya rangi ya bendera ya DRC, ambazo ni bluu, njano na nyekundu. Staili yake ya nywele na mawani vinamfanya kufanana kabisa na Hayati Lumumba.

Algeria yamtoa machozi

Katika mechi zote za DRC, Kuka hakuwa akishangilia wala kutikisika kwa dakika zote 90. Alifanya hivyo hadi timu yake ilipovuka hatua ya makundi.

Hata hivyo, Kuka alishindwa kujizuia katika mchezo wao wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Algeria, ambapo akiwa bado ameganda, alionekana akimwaga machozi.

Ni baada ya DRC kuruhusu bao pekee la dakika ya 119 lililowatoa kwenye mashindano hayo makubwa zaidi barani Afrika kwa ngazi ya soka la timu za taifa.

Alianza kitambo

Hata hivyo, wengi wamemfahamu kupitia fainali za AFCON zinazoendelea Morocco lakini Kuka alianza kufanya hivyo tangu mwaka 2023.

Akiwa na umri wa miaka 53 kwa sasa, Kuka amefichua kuwa kufanya kwake hivyo kunatokana na uzalendo mkubwa alionao kwa Taifa lake la DRC

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img