ANTALYA, Uturuki
Waziri wa Nishati, Dk. Juma Zuberi Homera, ameshiriki mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyewasili jijini Antalya, nchini Uturuki, Novemba 11, 2026, kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
Mkutano huo ni jukwaa muhimu kwa Tanzania kusukuma mbele vipaumbele vyake vya kimkakati katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuhamasisha upatikanaji wa takribani shilingi trilioni 7.3 kwa ajili ya kufadhili miradi ya mazingira inayolenga kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Rais Samia katika mkutano huo umebeba dhana isemayo: “Ushiriki Jumuishi wa Tanzania katika Kukabili Mabadiliko ya Tabianchi kuelekea Dira 2050: Kujenga Taifa Ustahimilivu, la Kijani na lenye Mafanikio.”
Katika mapokezi hayo, Wizara ya Nishati pia iliwakilishwa na Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi. Dk. Felchesmi Mramba.


