12.6 C
New York

Simba na mwendo wa kiume 2025

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

HAIKUWA rahisi. Simba imemaliza mechi zake za mwaka 2025 na sasa haitaonekana uwanjani hadi mwakani. Ilikuwa ni safari ndefu kweli kweli. Je, takwimu zinasemaje kwa mechi za Simba mwaka 2025? GAZETINI inakuchambulia kupitia makala haya. Endelea kusoma.

Ligi Kuu Bara

Simba kwa mwaka huu wamecheza mechi 20 za Ligi Kuu Bara. Katika michezo hiyo, ‘Wekundu wa Msimbazi’ wameshinda 15, wamefungwa miwili na sare mbili.

Mechi 15 ilizoshinda ni dhidi ya Mbeya City, JKT Tanzania (2), Namungo (2), Fountain Gate, Kagera Sugar, Ken Gold, Singida Black Stars, KMC, Pamba, Mashujaa, Dodoma Jiji, Coastal Union, Prisons na TRA.

Kwa mechi hizo, takwimu zinaonesha kuwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Bara wamefunga jumla ya mabao 47, pia eneo lao la ulinzi likiruhusu mabao tisa.

Kimataifa ilikuwaje?

Kwa upande wa kimataifa, Simba ilicheza jumla ya mechi 15, sita zikiwa za Ligi ya Mabingwa na tisa za Kombe la Shirikisho Afrika. Kati ya 15, walishinda sita, walifungwa minne na kutoa sare tano.

Mechi zao za ushindi kimataifa ni dhidi ya Nsingizini (3-0), Gaborone United (1-0), Stellenbosch (1-0), Al Masr (3-0), Constantine (2-0) na CS Safxien (1-0).

Kwa idadi ya mabao, Simba ya kimatafa imefunga mara 15, wakati huo ikiwa imeruhusu mara tisa.
Vipigo vikubwa zaidi.

Kwa mwaka 2025, Simba imepata ushindi mnono mara tatu; dhidi ya Ken Gold (5-0), Pamba (5-1) na Dodoma Jiji (6-0).

Pia, katika mechi zake 20 za mwaka 2025, Simba imepata ushindi wa 3-0 mara tisa dhidi ya Mbeya City, Nsingizini, Namungo (2), Fountain Gate, Al Masry, Prisons, na TRA.

FA ilikuwaje?

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho hapa nchini, Simba wameshinda mechi mbili kati ya tatu walizoshuka dimbani mwaka 2025.

Kama itakumbukwa, ushindi ulikuwa dhidi ya Mbeya City (3-1) na Bigman (2-1), huku Simba ikipoteza dhidi ya Singida Black Stars (3-1).

Kwamba katika mechi tatu, imefunga mabao nane, ingawa safu yake ya ulinzi imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara tano.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img