10 C
New York

Rais akamatwa, kushitakiwa kwa shutuma za rushwa

Published:

SUCRE, Bolivia

MWEZI mmoja tu baada ya kutoka madarakani, polisi nchini Bolivia wamemtia nguvuni Rais mstaafu, Luis Arce, ili kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Luis mwenye umri wa miaka 62, aliiongoza Bolivia kwa miaka mitano, kabla ya kumpisha, Rodrigo Paz aliyempiku katika Uchaguzi uliopita wa Oktoba, mwaka huu.

Kiongozi huyo anahusishwa na vitendo vya rushwa alipokuwa Waziri wa Uchumi kuanzia mwaka 2006 hadi 2019, kwa mujibu wa taarifa ya Serikali iliyotoka jana Desemba 10, 2025.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ulitawaliwa na hoja za kuporomoka kwa uchumi wa Bolovia, huku wananchi wengi wakitaka kufanyika kwa mabadiliko makubwa serikalini.

Akithibitisha kukamatwa kwa Luis, Makamu wa Rais, Edmand Lara amesema huyo ni mmoja ya mafisadi wanaosakwa na Serikali mpya ili kurejesha kila walichoiba wakiwa madarakani.

“Wale wote walioiba katika nchi hii, watarejesha kila walichochukua,” amesema Lara kupitia video yake katika mtandao wa TikTok.

Endapo Luis atakutwa na hatia katika mashitaka yaliyo mbele yake, atahukumiwa kifungo cha miaka minne au sita gerezani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img