9.5 C
New York

Mke wa rais kutupwa jela miaka 15?

Published:

SEOUL, Korea ya Kusini

WAENDESHA mashitaka wa Korea Kusini wameiomba Mahakama imuhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani aliyekuwa mke wa Rais wa zamani, Yoon Suk Yeol. Kim Keon Hee anakabiliwa na mashitaka mbalimbali, yakiwamo ya rushwa, ingawa amesema hajahusika katika hayo anayoshutumiwa nayo.

Wakati wa usikilizaji wa mashitaka yake jana, waendesha mashitaka waliiambia Mahakama kuwa Kim alijiingizia mamilioni ya fedha kwa njia za rushwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2011.

Aidha, walisema Kim alipewa rushwa ya vito vya thamani, ukiwamo mkufu wa dhahabu kutoka kwa Kanisa ili kulisaidia kupata msaada wa Serikali. Sambamba na kifungo, pia waendesha mashitaka wameomba Kim atozwe faini ya Dola za Marekani milioni 1.36.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img