9.8 C
New York

Mastaa EPL watakaoibukia AFCON 2025

Published:

CAIRO, Misri

MSIMU huu wa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) utaanza Desemba 21, mwaka huu, na kumalizika Januari 18, mwakani.

Kama ilivyo kawaida, fainali hizo huzipa maumivu klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) kwa baadhi ya wachezaji wake kurejea Afrika kujiunga na timu zao za taifa.

Hata hivyo, wakati klabu zingine zikiugulia, Arsenal, Chelsea na Leeds United hazitakumbana na maumivu kwani hazina wachezaji wa Afrika kwenye vikosi vyao.

Kwa upande mwingine, maumivu yatakuwa makali zaidi kwa Sunderland itakayopoteza wachezaji tisa watakaokwenda AFCON.

Nyota hao ni pamoja na Chemsdine Talbi (Morocco), Habib Diarra (Senegal), Simon Adingra (Ivory Coast) na Reinildo Mandava (Msumbiji).

Fainali za AFCON zitashirikisha mataifa 24, huku wenyeji Morocco wakipewa nafasi kubwa ya kulibakiza nyumbani taji la michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Ukiacha Sunderland, klabu zingine zitakazowakosa wachezaji muhimu kutokana na fainali hizo ni Manchester United, Bournemouth na Crystal Palace.

Kutokana na fainali hizo, Ruben Amorim atawakosa Bryan Mbeumo (Cameroon), Amad Diallo (Ivory Coast) na Noussair Mazraoui (Morocco).

Liverpool, pigo pekee kwa kocha wake, Arne Slot, ni kumkosa Mohamed Salah atakayerejea Misri kuiwakilisha timu yake ya taifa ya Misri kwenye michuano hiyo.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, naye atakumbana na maumivu ya kumkosa mshambuliaji wake raia wa Misri, Omar Marmoush.

Tottenham, kwa upande wao, watawakosa wachezaji wake muhimu wawili, ambao ni Yves Bissouma (Mali) na Pape Matar Sarr (Senegal).

Baadhi ya mastaa wengine wa EPL watakaorejea Afrika ni Evann Guessand (Aston Villa, Ivory Coast), Dango Ouattara (Brentford, Burkina Faso) na Carlos Baleba (Brighton, Cameroon).

Wengine ni Axel Tuanzebe (Burnley, DRC), Ismaila Sarr (Crystal Palace, Senegal), Iliman Ndiaye na Idrissa Gueye (Everton, Senegal), Alex Iwobi (Fulham, Nigeria).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img