21.7 C
New York

Vinicius ataka mshahara wa Mbappe

Published:

MADRID, Hispania
KWA mujibu wa kile kilichoripotiwa na Gazeti la Sport la Hispania, Vinicius Jr anataka alipwe mshahara sawa na Kylian Mbappe ili kubaki Real Madrid.
Vinicius mwenye umri wa miaka 25, anaamini kwa kiwango chake, hastahili kuzidiwa mshahara na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Kwa miezi kadhaa sasa, mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Vinicius na Madrid yameshindwa kuendelea, hiyo ikitokana na pande mbili hizo kushindwa kukubaliana.
Inaelezwa kuwa mabosi wa Madrid, licha ya kuheshimu kiwango bora cha Mbrazil, hawako tayari kukubaliana na mshahara anaoutaka.
Hata hivyo, zipo taarifa kuwa Vinicius hafurahishwi na namna anavyochukuliwa na kocha mpya, Xabi Alonso.
Nje ya Madrid, zipo klabu za Saudi Arabia zinazomtolea macho na inasemekana kuwa zimetenga dau nono kumsajili ifikapo mwakani.

Related articles

Recent articles