6.4 C
New York

Nana Miriam awaonjesha mashabiki ‘C’est Jesus’

Published:

Na MWANDISHI WETU

MWIMBAJI anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili nchini Kongo, Nana Miriam ameachia kionjo cha wimbo mpya, C’est Jésus, alioshirikiana na Sylvain Kashila.

Waimbaji hao ambao kwasasa ni tishio nchini Kongo, wameteka hisia za mashabiki wa muziki huo punde baada ga kuachia kionjo cha ngoma hiyo inayotarajia kutoka Novemba 16, mwaka huu.

Akizungumzia kolabo hiyo Nana Miriam, amewataka mashabiki wa Afrika Mashariki na Kati wakae mkao wa kumtukuza Mungu kupitia wimbo huo uliowabariki wengi.

“Wimbo unatoka wiki ijayo Novemba 16, naomba mashabiki zetu wa hapa Kongo, Tanzania na sehemu nyingine dunia wakae karibu na mitandao yetu ya kijamii ili video inapotoka waweze kutupa sapoti ili kolabo yetu hii C’est Jésus ifike mbali,” amesema Nana.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img