LAGOS, Nigeria
SUPASTAA wa Afrobeats, Burna Boy, amemtaja Jay Jay Okocha kuwa ndiye mchezaji wake bora, akiwatupa kando Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Burna Boy amesema yeye si shabiki wa Ronaldo wala Messi, licha ya dunia kuwataja zaidi wawili hao.
“Nitasema Jay Jay Okocha. Ni kati yake na Pele. Sipo katika mijadala ya Ronaldo na Messi,” amesema mwanamuziki huyo katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha ESPN.
Kwa upande mwingine, Burna Boy amefunguka kuwa yeye ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Manchester United.
Aidha, mshindi huyo wa tuzo ya Grammy amesema Lamine Yamal ndiye kinda bora kwa upande wake, ingawa Kobbie Mainoo naye anafanya vizuri.


