5.7 C
New York

Halopesa yatoa msaada wa viti mjongeo Hospitali ya Mwananyamala

Published:

Na Imani Nathanieli

Katika kuadhimisha miaka tisa, Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel kupitia huduma ya kifedha ya Halopesa, imetoa msaada wa viti mjongeo 15 kwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaama.

Msaada huo ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo katika kusaidia sekta mbalimbali za kijamii, ambapo kwa sasa wanaasema wameelekeza nguvu katika sekta ya afya, ikiwa ni njia ya kuimarisha ustawi wa jamii.

Mkurugenzi wa Halopesa, Nghien Anh Thong, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, amesema wanajivunia kuwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya jamiii ya watanzania.

” Hili ni jambo la faraja kubwa kwetu. kupitia Halopesa, tuna dhamira ya dhati kusaidia sekta ya afya kwa kuwafikia wahitaji,”amesema Thong.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi , Magesa Wandwi, alieleza kuwa miaka tisa ya kampuni ni mafanikio makubwa yanayoashiria ushirikiano imara na jamii.

“Maadhimisho haya ni ushindi wa uhusiano wetu na jamii. Tunaamini mafanikio ya kweli hupatikana pale tunapoweza kushiriki kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu,” ameeleza.

Naye Ofisa Masoko wa Halopesa, Aidat Lwiza, amesema si huduma ya kifedha pekee bali ni taasisi inayowekeza katika maendeleo ya kijamii.

“Mafanikio ya kibiashara yanakuwa na thamani kubwa zaidi pale yanapowaletea jamii matokeo chanya. Tunaamini katika kufanya biashara kwa kuwajali watu,” amesema.

Mratibu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamara, Lilian Kokushubiramwanga, ametoa shukrani kwa mchango huo na kusema kuwa umekuja wakati sahihi wakiwa katika mazingira ya uhitaji mkubwa wa vifaa tiba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img