9.5 C
New York

Halopesa yaja na kampeni ‘Tamba na Bonasi’

Published:

Na Imani Nathaniel, Gazetini

Kampuni ya Halotel kupitia huduma yake ya kifedha Halopesa imezindua kampeni mpya inayokwenda kwa jina la “Tamba na Bonasi”, ili kuwazawadia wateja wake bonasi na zawadi mbalimbali kulingana na miamala wanayofanya kila siku.

Kampeni hiyo imezinduliwa leo Septemba 19,2025 jijini Dar es Salaam na inakuja sambamba na utambulisho wa msaidizi wa kidigitali anayefahamika kama Mr. Bonasi, ambaye atavaa sura rasmi ya kampeni.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Idara ya Biashara wa Halotel, Happy Mzena, amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kutoa motisha kwa wateja kwa kuwazawadia zawadi za pesa taslimu hadi sh 2,000,000, kupitia droo za kila siku, kila wiki, na kila mwezi.

Amesema ili kuingia katika droo, mteja anapaswa kufanya miamala kupitia Halopesa kama vile kutoa pesa, kulipia bidhaa, au kununua LUKU.

“Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wetu wa kuendelea kuwapa wateja thamani zaidi. Mr. Bonasi siyo tu nembo ya kampeni, bali ni jukwaa la kidigitali la zawadi linaloleta msisimko katika kila muamala. Lengo letu ni kuifanya kila huduma ya Halopesa kuwa fursa ya ushindi kwa wateja wetu,” amesema Mzena.

Kwa upande wake, Ofisa Masoko wa Halopesa, Aidat Lwiza, ameeleza kuwa kampeni hiyo imeandaliwa kwa ubunifu mkubwa na inaleta thamani halisi kwa mteja.
Aliongeza kuwa Halopesa inaendelea kushikilia nafasi ya juu katika soko kwa kutoa gharama nafuu zaidi kwa miamala pamoja na mtandao mpana wa mawakala na maduka kote nchini.

“Tunawakaribisha Watanzania wote kujiunga na Halopesa, kwani kwa sasa kila muamala siyo tu njia ya kutuma au kupokea fedha, bali ni hatua moja kuelekea ushindi,” amesema Aidat.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img