MERSEYSIDE, England
LIVERPOOL ndiyo klabu ya Ligi Kuu ya England iliyotumia fedha nyingi zaidi wakati wa dirisha kubwa la usajili wa kiangazi barani Ulaya.
Usajili huo uliofungwa hivi karibuni, uliishuhudia Liverpool ikitumia Pauni milioni 426.
Chelsea inashika nafasi ya pili kwa Pauni milioni 263, ikifuatiwa na Newcastle United iliyomwaga Pauni milioni 249.
Arsenal inafuata ikiwa na Pauni milioni 241, wakati Manchester United iko nafasi ya tano kwa matumizi ya Pauni milioni 215. Manchester City iliyotumia Pauni milioni 176 na kushika nafasi ya saba, imejikuta ikizidiwa na Nottingham Forest iliyokaa juu yake.
Kwa upande mwingine, Aston Villa ndiyo timu iliyokuwa na bajeti ndogo zaidi, ikitumia Pauni milioni 40.


