11.6 C
New York

Trump amshambulia Obama, ataka ashitakiwe

Published:

WASHINGTON, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amemtaja mtangulizi wake, Barack Obama, kuwa ni muhaini na anayepaswa kufunguliwa mashitaka.
Kwa mujibu wa Rais Trump, Obama alishirikiana na Urusi kuendesha kampeni za kumchafua na kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2016.
Wakati huo huo, amesema mtangulizi wake huyo aliratibu njama za kuharibu kampeni zake katika Uchaguzi huo.
Aidha, Rais Trump ameenda mbali zaidi na kutishia kuukabidhi utawala wa Obama kwa waendesha mashitaka, akidai ulishirikiana na Urusi kuuvuruga Uchaguzi huo.
Gabbard alisema zipo nyaraka zikionesha namna viongozi wa juu wa Serikali ya Obama walivyohusika ‘kumchezea rafu’ Trump alipokuwa akiwania kiti cha urais.
Rais Trump akisisitiza katika hilo, alisema: “Ushahidi upo, ana hatia. Huu ulikuwa ni uhaini. “Walijaribu kuiba Uchaguzi, walijaribu kuutibua chaguzi. Walifanya kitu ambacho si rahisi kuamini.”
Hata hivyo, kambi ya Obama imeibuka na kukanusha madai hayo, ikiyaita kuwa ni uzushi usiopaswa kupewa nafasi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img