11.6 C
New York

Waasi waua sita, wateka 100 Nigeria

Published:

MAIDUGURI, Nigeria
KATIKA tukio lililotokea jana, kundi la waasi limevamia na kuuua watu sita, huku likiondoka na wengine zaidi ya 100, wakiwamo watoto na wanawake.
Taaria zinaeleza kuwa watu wenye silaha walivamia Kijiji cha Kairu, Kaskazini-Magharibi mwa Jimbo la Zamfara.
Zamfara ni kitovu cha vikundi vya waasi Kaskazini mwa Nigeria, ambapo matukio ya mauaji na utekaji wa raia yamekuwa ya kiwango cha juu katika miaka ya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Hamisu Faru ambaye ni mkazi wa eneo hilo, wakazi wengi wa eneo hilo wamelazimika kuyakimbia maeneo yao wakihofia vikundi hivyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img