KINSHASA, DRC
SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) itakaa mezani na M23 kusaini mkataba wa kumaliza vita Kaskazini mwa nchi hiyo.
Hatua hiyo ni mafanikio ya mazungumzo ya miezi kadhaa yaliyosimamiwa na Qatar.
Mkataba huo utasainiwa leo mjini Doha, pia ikikumbukwa kuwa Marekani ilikuwa na nguvu kubwa katika kushawishi pande mbili hizo kufikia makubaliano.
Kwa mujibu wa taarifa, Marekani inasubiri kuona amani ikirejea eneo hilo ili ianze kuwekeza katika sekta ya madini.
M23 inayotajwa kupewa nguvu na Rwanda, imeweka makazi ya Goma, ambao ndiyo Mji mkubwa zaidi kwa upande wa Mashariki mwa DRC.
Mwaka huu pekee umeshuhudia vita kati ya wanajeshi wa Serikali na M23 imesababisha mauaji ya maelfu ya raia
Machi, mwaka huu, Qatar ilisimamia mazungumzo ya kusaka amani kati ya Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye amekuwa akishutumiwa kushirikiana na M23.
Itakumbukwa kuwa mazungumzo hayo ndiyo yaliyojenga msingi wa yale ya DRC kukaa mezani na M23 mjini Doha.
Published:


