11.6 C
New York

Jeshi laifuta Tume cha Uchaguzi Burkina Faso

Published:

OUAGADOUGOU, Burkina Faso
UTAWALA wa kijeshi nchini Burkina Faso umeifuta iliyokuwa Tume ya Uchaguzi kwa madai kuwa uwepo wake ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Serikali, shughuli zote za Uchaguzi sasa zitasimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Tangu jeshi lilipojitwalia madaraka mwaka 2022 na Ibrahim Traore kuingia Ikulu, limefanya mabadiliko kadhaa, ikiwamo kusogeza mbele Uchaguzi Mkuu.
Kama itakumbukwa, ulipaswa kufanyika mwaka jana lakini sasa utafanyika Julai,2029.
Hatua ya kuifuta Tume ya Uchaguzi imebebwa na hoja kwamba ilikuwa ikitumia zaidi ya Dola 870,000 kwa mwaka.
kwa muda sasa, utawala wa wa kijeshi nchini humo umekuwa ukipingwa na jumuhiya za kimataifa, ukitajwa kukiuka haki za binadamu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img