MOSCOW, Urusi
MAHAKAMA nchini Urusi imemuhukumu kifungo cha miaka 14 gerezani mwandishi wa vitabu,
Boris Akunin, kwa kauli yake ya kuiunga mkono Ukraine.
Pia, mbali ya kuiunga mkono Ukraine ambayo ni ‘adui’ wa Urusi, pia Akunin alishinikiza mapinduzi ya kumuondoa madarakani Rais Vladimir Putin.
Mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 69, amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Urusi, hasa kwa hatua yake ya kuwavamia kijeshi majirani zao, Ukraine.
Kutokana na ukosoaji wake, mamlaka za Urusi zilishamuweka Akunin katika orodha ya magaidi na ‘mawakala wa maadui wa nje’.
Hata hivyo, hukumu dhidi yake imetafsiriwa kuwa ni mwendelezo wa Serikali ya Putin ‘kuwanyoosha’ wakosoaji wake.
Ukiacha waliolazimika kukimbilia nchi zingine, waliobaki wameishia kukamatwa na kuteswa na vyombo vya dola.
Published:


