11.6 C
New York

Al Shabaab wateka mji Somalia

Published:

MOGADISHU, Somalia
WANAMGAMBO wa Al Shabaab wameuteka na sasa wameweka makazi katika Mji wa Tardo mkoani Hiiran.
Tardo ni Mji ulio katikati ya Somalia, hivyo unaipa Al Shabaab nafasi ya kusogea kirahisi katika maeneo mengine.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Somalia, maelfu ya wakazi wa eneo hilo wamelazimika kukimbia.
Hatua hiyo ya Al Shabaab kuupata Mji huo mwishoni mwa wiki iliyopita ilitanguliwa na mapambano makali na jeshi la Somalia.
Al Shabaab wamekuwa wakiitesa Somalia tangu mwaka 2007, lengo lao kubwa likiwa ni kuiondosha Serikali na kuweka utawala utakaoongoza kwa misingi ya sheria za Uislam (Sharia).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img