11.6 C
New York

Rais Biya ataka muhula wa nane Cameroon

Published:

YAOUNDE, Cameroon
RAIS wa Cameroon, Paul Biya, ametangaza nia ya kugombea tena katika Uchaguzi Mkuu ujao, licha ya kwamba ameshika nafasi hiyo kwa miaka 43.
Biya mwenye umri wa miaka 92, amesema anavutiwa kugombea tena kwa kuwa anaona bado ana mengi ya kuifanyia Cameroon.
“Kuna mengi ya kufanya na kuna mazuri mengi yanakuja,” amesema Biya katika taarifa yake ya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Biya ametangaza nia hiyo kuelekea Uchaguzi wa Oktoba, licha ya taarifa kudai kuwa anapitia changamoto za afya.
Huku taarifa za kuzorota kwa afya yake zikiendelea, ziliwahi kuibuka pia zile zilizodai kuwa kiongozi huyo amefariki.
Aidha, Biya amedai uamuzi wake wa kugombea umetokana na maombi aliyopokea kutoka katika mikoa 10, pamoja na raia wa Cameroon wanaoishi nje ya nchi.
Aliingia madarakani mwaka 1982 na anakuwa mmoja ya viongozi wa Afrika walioongoza muda mrefu.
Kwa upande mwingine, Biya ni rais wa pili kuiongoza Cameroon tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Ufaransa mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img