9.8 C
New York

Urusi yaishambulia Kyiv, yaua wawili

Published:

KYIV, Ukraine
WATU wawili wameripotiwa kufariki katika shambulizi la Urusi mjini Kyiv, Ukraine.
Ndege isiyo na rubani iliishambulia Kyiv, ikielezwa pia watu 13 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na mamkala za Kyiv, ndege hiyo ilishambulia jengo la makazi ya raia katika Wilaya ya Shevchenkivskyi.
Aidha, kabla ya hilo, usiku wa Jumanne ya wiki hii, Ukraine ilieleza kupata shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu ilipoingia katika mgogoro wake na Urusi.
Katika shambulio hilo, ndege zisizo na rubani zipatazo 728 zilishambulia miji mbalimbali ya Ukraine.
Ni katika matukio hayo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine, Ihor Klymenko, alisema ofisa wa polisi mwenye umri wa miaka 22 alipoteza maisha.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img