9.8 C
New York

Marekani yambana mbavu mjumbe UN

Published:

NEW YORK, Marekani
SERIKALI ya Marekani chini ya Rais Donald Trump imemwekea vikazo mjumbe wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UN), Francesca Albanese.
Hatua hiyo imekuja huku ikifahamika wazi kuwa Albanese amekuwa mkosoaji mkubwa wa mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani, Marco Rubio, vikwazo alivyowekewa Albanese vinahusisha kuzuiwa kuingia Marekani.
Pia, mali zake zilizoko Marekani zitazuiwa, sambamba na kutoweza kujihusisha moja kwa moja na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Rubio amemshutumu Albanese akimtaja kuwa ni mkosoaji wa wazi wa Marekani na Israel, pia anayeunga mkono matukio ya ugaidi.
Kwa upande wake, Albanese amelaani adhabu hiyo ya Marekani akiita kuwa ni mbinu za ‘kimafia’ dhidi yake.
Aidha, wengi wanakumbuka kuwa Marekani imekuwa kwenye vita kali dhidi ya ICC tangu mwaka jana, baada ya Mahakama hiyo ilipotaka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akamatwe.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img