NEW YORK, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amekiri kuwa haoni kama atafanikiwa kuimaliza vita inayoendelea kati ya mataifa ya Ulaya Mashariki, Urusi na Ukraine.
Hata hivyo, Rais Trump ameweka wazi kuwa ni matamanio yake kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miezi kadhaa sasa.
Katika kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu uliomrudisha madarakani, mwanasiasa huyo aliahidi kumaliza vita hiyo, akiutaja mpango huo kuwa ni kipaumbele chake mara tu atakapoingia Ikuku.
Jitihada za awali zilimshuhudia Rais Trump akifanya mazunguzo ya simu na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, pia akizungumza kwa njia hiyo na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr .
Lakini, licha ya mazungumzo ya Zelenskyy kutajwa kwenda vizuri, vyombo vya habari vilieleza kuwa haikuwa hivyo kwa upande wa Putin.
Alipoulizwa juu ya uwezekano wa kutimiza. ndoto ya ‘kuzika’ uhasama kati ya Urusi na Ukraine, Rais Trump alisema:
“Sijui. Siwezi kusema ndiyo au hapana. Siwezi kutabiri kitakachotokea,” alisema Rais Trump na kusisitiza kuwa bado kipaumbele chake ni kurejesha amani kati ya mataifa hayo.
Published:


