5.5 C
New York

Miquissone aibipu Simba, atayaweza?

Published:

Na Winfrida Mtoi, Gazetini

BAADA ya Simba kupoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, winga wa zamani wa timu hiyo raia wa Msumbiji Luis   Miquissone  ameandika kwenye istagram yake  kama anauliza swali ‘Nirudi au vip uko’.

Simba imepoteza kwa kufungwa nyumbani na Petro de Luanda ya Angola bao 1-0 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Utani alioandika mchezaji huyo aliyewahi kufanya makubwa Msimbazi inaonekana bado anatamani kurejea katika kikosi hicho ambapo kwa sasa anakipiga US Dongo ya nchini kwao Msumbiji.

Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Luis alitua Simba mwaka 2020 na alisajiliwa kwa dau kubwa kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini licha ya kwamba kipindi hicho alikuwa akicheza kwa mkopo UD Songo.

Fedha waliyotoa Simba kipindi hicho kunasa saini ya mchezaji huyo haikwenda bure kwani  ililipa ndani ya kipindi kifupi baada ya nyota huyo kuwa lulu na  kupata ofa ya kujiunga na Al Ahly ya Misri mwaka 2021 ambayo ilitoa kitika cha maana kumnunua mchezaji huyo.

Hata hivyo alishindwa kuwika katika kikosi cha Al Ahly hali iliyofanya apelekwe kwa mkopo Abha Club ya Saudi Arabia, kisha msimu 2023/2024 Simba ilimrejesha Msimbazi, lakini hakuonesha makali kama mwanzo, hivyo kuamua kuachana naye.

Kutoka na alichoandika nyota huyo katika Instagram yake, je kwa hali ya kikosi cha Simba kwa sasa anaweza kupata nafasi na kufanya vizuri? Katika maoni ya baadhi ya mashabiki wanayotoa baada ya kuandika ujumbe huo, wapo wanamsapoti, huku wengine wakimkataa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img