21.7 C
New York

Kashfa BBC| Mkurugenzi Mkuu, CEO waachia ngazi

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Tim Davie, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kufuatia lawama nzito zilizotokana na madai kuwa kipindi cha uchunguzi cha Panorama kilihariri vibaya hotuba ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na hivyo kupotosha watazamaji.

Sambamba na Davie, Deborah Turness, ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Habari za BBC (CEO of BBC News), naye ametangaza kuachia wadhifa wake kutokana na sakata hilo ambalo limezua mjadala mkubwa kuhusu uadilifu wa taarifa na uaminifu wa vyombo vya habari.

Deborah Turness (pictured), chief executive of BBC News, also resigned, saying the ‘buck stops with me’
Deborah Turness, ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Habari za BBC (CEO of BBC News).

Tim Davie, ambaye amehudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa BBC kwa kipindi cha miaka mitano, amekuwa akikabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na misururu ya migogoro ya ndani na malalamiko kuhusu usimamizi wa maadili ya uhariri ndani ya shirika hilo la utangazaji lenye heshima kubwa duniani.

Akizungumza Jumapili jioni wakati akitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu, Davie alisema:

“Kama taasisi ya umma, BBC siyo kamilifu. Tunapaswa daima kuwa wazi, wawazi na wawajibikaji. Kwa ujumla BBC inafanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake, lakini kumekuwa na makosa yaliyofanyika, na kama Mkurugenzi Mkuu, ni wajibu wangu kubeba dhamana ya mwisho.”

Tuhuma hizi zimeibua maswali makubwa kuhusu uhariri na uwajibikaji wa vyombo vya habari vya umma, hususan katika nyakati ambapo usahihi wa taarifa ni muhimu kwa uaminifu wa wananchi.

Hadi sasa, bodi ya BBC haijatangaza nani atakaekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu, huku wachambuzi wa masuala ya habari wakitaja kujiuzulu kwa Davie kama “hatua muhimu katika kurejesha imani ya umma kwa shirika hilo”.

Davie aliteuliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2020, akiwa amejikita katika kuimarisha utoaji wa huduma za kidijitali na kulinda uhuru wa uhariri, lakini amekumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo migogoro ya ndani kuhusu uhalisia wa maudhui na mabadiliko ya kiutendaji ndani ya shirika hilo lenye historia ndefu.

Tim Davie.

Related articles

Recent articles