5.7 C
New York

Mabosi Mwendokasi wang’olewa

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa mabosi wapya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) maarufu Mwendokasi kwa kuwaondoa Mtendaji  Mkuu Dk. Athuman Kihamia na  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya UDART, Waziri Kindamba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga, walioteuliwa ni Said Tunda anayechukua nafasi ya Dk. Kihamia na  Pius Ng’ingo anayechukua nafasi ya Waziri Kindamba.

Uteuzi huo unakuja siku moja baada ya wananchi kufanya fujo kwa kupiga mawe mabasi hayo jana katika maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam kutokana na kuchoshwa na hali ya usafiri  huo.

Wakati uteuzi huo unafanyika tayari mabasi mapya yameanza kufanya kazi katika njia  ya Kimara, Gerezani,  Kivukoni na Morocco.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img