13.9 C
New York

Makamu wa Rais Sudan afunguliwa mashitaka

Published:

JUBA, Sudan Kusini
MAKAMU wa Rais wa Kwanza wa Sudan Kusini, Riek Machar, amefunguliwa mashitaka akishutumiwa kwa uhaini na mauaji.
Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria, Joseph Geng Akech, mashitaka dhidi ya Machar yanatokana na kuhusika kwake katika machafuko ya Machi, mwaka huu.
Hata hivyo, mashitaka hayo yanaibua hofu ya kuibuka upya kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini.
Ikumbukwe, wapiganaji waliokuwa wakimuunga mkono Machar waliingia vitani kwa miaka mitano dhidi ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir, kabla ya pande mbili hizo kumaliza tofauti zao mwaka 2018.
Mkataba huo wa amani ulihitimisha vita iliyosababisha vifo takribani 400,000. Machar amekuwa chini ya ulinzi tangu Machi, mwaka huu, sambamba na washitakiwa wengine saba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img