13.9 C
New York

Rais ahukumiwa miaka 27 gerezani

Published:

RIO, Brazil
RAIS wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu gerezani kwa kosa la kusuka mpango wa kupindua Serikali iliyoko madarakani.
Bolsonaro anatajwa kujihusisha na mpango huo baada ya kushindwa kwenye boksi la kura na aliyekuwa mpinzani wake, Luiz Inácio Lula da Silva, katika Uchaguzi wa mwaka 2022.
Kwa upande wao, wanasheria waliokuwa wakimtetea wamesema hukumu hiyo ni ukatili dhidi ya mwanasiasa huyo na wameahidi kukata rufaa.
Kabla ya hukumu, Bolsonaro aliwahi kujibu shutuma hizo akisema zimelenga kumzuia kugombea katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2026.
Ifahamike kuwa Bolsonaro ni mshirika mkubwa wa Marekani na mashitaka yake yanatajwa kusababisha Rais Donald Rrump kuzipandishia ushuru kwa asilimia 50 bidhaa zote za Brazil zinazoingia nchini humo.
Hata baada ya hukumu, Katibu Mkuu wa Marekani, Marco Rubio, ameahidi Taifa lake kuchukua hatua dhidi ya Brazil akisema Mahakama Kuu haikutenda haki dhidi ya Bolsonaro.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img