15.5 C
New York

Chanzo machafuko yanayoendelea Yemen

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
KUNDI la waasi la Houthis limeendelea kuwateka wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (UN) wanaoingia nchini Yemen humo kwa ajili ya kuwasaidia raia kipindi hiki cha vita.
Januari, mwaka huu, wafanyakazi nane wa UN walitekwa baada ya wengine 25 waliokuwa wanashikiliwa na Kundi hilo tangu mwaka 2023 kuachiwa.
Kama hiyo haitoshi, hivi karibuni, kundi hilo linaloshikilia maeneo mengi ya Yemen, lilivamia ofisi za UN mjini Sanaa na kuteka wafanyakazi saba wa Umoja huo, pamoja na kuondoka na nyaraka mbalimbali.
Hatua hiyo ilikuja baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni kukarishwa na shambulizi la bomu lililofanywa na Israel katika makao makuu ya Serikali ya Kundi hilo mjini Sanaa.
Kupitia taarifa yao baada ya tukio hilo, kiongozi wa kijeshi wa Houthis, Abdul Malik al-Houthi, alijipaza kutokufumbua machozi na kuahidi jitihada za makusudi za kulipa kisasi.
Ikumbukwe, tangu mwaka 2023, Yemen imeshuhudiwa ikiwa na mapigano makali kati ya Houthis na wanajeshi wa Israel.
Katika shambulizi la Agosti 28, mwaka huu, shambulizi la Israel lilisababisha kifo cha Waziri Mkuu wa Serikali ya Houthi, Ahmed Ghalib al-Rahawi, na viongozi wengine 11, akiwamo Waziri wa Michezo.
Licha ya kutokuwa sehemu ya jeshi, al-Rahawi, alikuwa mtu muhimu ndani ya Kundi hilo na kifo chake kimetajwa kuwa ni pigo kubwa kwa Houthi.
Houthis wanaojinasibisha na sheria za Dini ya Uislam (Sharia), wamekuwa chanzo cha hali mbaya ya usalama nchini Yemen kwa miaka zaidi ya 20 ya hivi karibuni.
Vita vyao ni dhidi ya Serikali iliyoko madarakani, ambayo ndiyo inayotambulika kimataifa ikiungwa mkono pia na Saudi Arabia.
Hata hivyo, licha ya ushindani mkubwa kutoka kwa Saudi Arabia na mataifa mengine, Houthis imefanikiwa kutawala Kaskazini mwa Yemen, ukiwamo Mji Mkuu wa Sanaa. Wapinzani wao wanashikilia maeneo ya Kusini.
Mgogoro huo umesababisha watu takribani milioni 21 kuwa kwenye uhitaji mkubwa wa misaada, kwa mujibu wa ripoti ya UN.
Kwa upande wake, mchambuzi wa siasa wa Yemen, Mohammed al-Basha, anaamini hatua ya Kundi hilo kuwateka wafanyakazi wa UN ni mwanzo tu.
“Huenda operesheni zao zikaingia hata kwenye asasi za kiraia za kimataifa (INGO), balozi za kigeni, taasisi za fedha na maduka ya kubadilisha fedha,” anasema Al-Basha.
Mwandishi wa habari wa Yemen, Adnan al-Jabarni, anasisitiza kuwa Kundi hilo linawashikilia raia takribani kuanzia mwaka 2018 hadi 2025 kwa madai ya kushirikiana na taasisi za kimataifa.
“Wamewafunga jela watu wengi mjini Sanaa, wakiwamo hata baadhi ya viongozi katika Kundi hilo. Ni kama wana wasiwasi kuwa kuna wanaovujisha siri zao,” anasema Al-Jabarn.
Hata hivyo, wakijibu tuhuma za kuwaweka mafichoni wafanyakazi 34 wa UN, Houthis wanasema watu inaowashikilia ni wale tu iliojiridhisha kuwa ni wapelelezi wa Marekani na Israel.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img