6.4 C
New York

Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga kuanzia Angola, Simba Botswana

Published:

Na Mwandishi Wetu

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga itaanza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola wakati Simba itacheza na Gaborone United ya Botswana.

Wababe  hao wa Tanzania Bara wote wataanzia ugenini kati ya Septemba 19 na 21, 2025 na kurudiana kati ya Septemba 26 na 28, 2025 jijini Dar es Salaam.

Yanga ikipita hatua hiyo itakutana na mshindi  wa mchezo kati ya Algeci Plus ya Madagascar dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, huki Simba ikivuka hatua itacheza na mshindi wa mchezo wa Bhora ya Zimbabwe na Nsingizia Hotspurs ya Eswatin.

Wawakilishi wa Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya  Mlandege itaanzia ugenini   ikicheza na  Insurence ya Ethiopia.

Kwa upande wa  Kombe la Shirikisho Azam FC itaanzia nyumbani dhidi ya El Merrekh Bantiu ya Sudan Kusini,  Singida Bs  wamepangwa kucheza na Rayon Sports ya Rwanda, wakati KMKM ya Zanzibar  itacheza na AS Port ya Djibouti ambapo zote zitaanzia ugenini.

Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho imefanyika leo Agosti 9, 2025 jijini Dar es Salaam na kushudiwa na viongozi mbalimbali wa soka hapa nchini na Afrika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img