9.3 C
New York

Magenge ya uhalifu yanavyoitesa Serikali ya Mexico – [1]

Published:

SINALOA, Mexico

HIVI karibuni, Shirika la Ujasusi la Marekani [FBI] lilimtia nguvuni binadamu aitwaye Fausto Isidro ‘Chapo Isidro’.

Kwa wasiomfahamu, Chapo Isidro ni miongoni mwa wamiliki wa magenge ya mtandao wa biashara ya ‘unga’ nchini Mexico.

Kama hiyo haitoshi, Chapo Isidro [44], alikuwa sehemu ya orodha ya wahalifu 10 waliokuwa wakisakwa kwa miaka mingi na FBI kutokana na ushiriki wake kwenye biashara hiyo ndani na nje ya Mexico.

Kwanini Wamarekani walimsaka? Ni kwa sababu Chapo Isidro alikuwa akisafirisha kwa wingi dawa hizo kuingia nchini kwao, kama ilivyo kwa wenzake wanaofanya biashara hiyo Mexico na Amerika ya Kusini kwa ujumla.

Hata hivyo, haikuwa rahisi kumdaka Chapo Isidro. Miaka yote aliyotafutwa, alikuwa akijificha na wakati mwingine kujichanganya mitaani akiwa kwenye maisha ya kawaida ili kutojulikana.

Hata hivyo, baada ya kunasa taarifa za alikojificha mjini Sinaloa, vyombo vya dola vya Mexico vikishirikana na FBI vilitumia helikopta kufanya shambulizi la kushitukiza.

Katika masambulizi makali hayo, walinzi saba wa Chapo Isidro waliripotiwa kuuawa, huku wengine nane wakiishia mikononi mwa makomandoo wa Mexico na Marekani.

Miongoni mwa waliokamatwa ni binadamu yake, ambaye ndiye mtu wa pili kwa ushawishi ndani ya kundi baada ya Chapo Isidro.

Pia, zipo taarifa za kuaminika zinazodai kuwa mwingine aliyekamatwa ni shimeji yake, ambaye alikuwa akiongoza idara ya fedha kwenye Kundi hilo.

Mexico inayoongozwa na Rais Claudia Sheinbaum, imelazimika kuendesha opresheni kali dhidi ya magenge ya uhalifu wa dawa za kulevya, zikiwamo heroine na cocaine, baada ya shinikizo kali kutoka kwa Donald Trump.

Kwa wasiomfahamu, Chapo Isidro amekuwa akiliongoza genge maarufu la ‘Meza Flores Organisation’, maarufu pia kwa jina la ‘Guasave Cartel’, tangu miaka ya 1990.

Jina la Chapo Isidro liliingia kwenye orodha ya wahalifu 10 wanaotafutwa zaidi na FBI mwaka 2025. Ni baada ya kujizolea umaarufu kwa shughuli za kuuza unga, kuteka na kutesa watu.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa FBI wakati huo, Brian Driscoll, alisema Chapo Isidro amekuwa akiingiza kiwango kikubwa cha dawa za kulevya nchini Marekani akitumia mpaka wao na Mexico.

Mwaka 2012, Marekani ilimfungulia mashitaka ya dawa za kulevya, ikiwamo bangi, kabla ya kumpa tena kesi ya aina hiyo mwaka 2019.

Historia inakumbusha kwamba aliwahi kuwa kiongoni mwandamizi wa genge la uhalifu la Beltran Leyva Organization na lilipovunjika ndipo akaanzisha lake mwaka 2013.

Lakini, kwa upande mwingine, Chapo Isidro ni mfano mdogo tu wa tatizo kubwa la magenge ya uhalifu yanavyoitesa nchi ya Mexico.

Itaendelea …

Related articles

Recent articles