10.6 C
New York

Mahakama yamchomoa gerezani Waziri Mkuu

Published:

SEOUL, Korea ya Kusini

MAHAKAMA Kuu ya Korea ya Kusini imeipangua hukumu ya kifungo cha miaka 15 gerezani aliyokuwa nayo Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Han Duck-soo.

Duck-soo alihukumiwa kwa kuhusika kwake katika sheria iliyotaka jeshi kushika dola mwaka 2024, wakati huo Korea ya Kusini ikiwa chini ya Yoon Suk Yeol.

Katika hukumu yake, Mahakama Kuu imejiridhisha kuwa waendesha mashitaka hawakuwa na Ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mwanasiasa huyo.

Baada ya Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo, kesi sasa itarudi katika hatua ya awali, kwa maana ya Mahakama iliyokuwa imemfunga Mei, 2026.

Kipindi hicho pia, Mahakama ilimfunga miaka minne mke wa Waziri Mkuu huyo, Kim Keon Hee, aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka mbalimbali, yakiwamo ya rushwa.

Related articles

Recent articles