11.8 C
New York

Mchungaji aliyemuua Rais asubiri kifungo cha maisha

Published:

FLORIDA, Marekani

MCHUNGAJI wa kanisa mjini Florida, Emmanuel Sanon, amekutwa na hatia kati ya kesi ya mauaji ya Rais wa Haiti, Jovenel Moise.

Aidha, mchungaji huyo amekutwa na hatia zikiwa Sanon baada ya kesi yake kuunguruma kwa takribani wiki nane.

Sanon, raia pacha wa Marekani na Haiti mwenye umri wa miaka 67, anasubiri hukumu ya kifungo cha maisha gerezani.

Kwa mujibu wa taarifa, alishitakiwa kwa kusuka mpango wa mauaji ya Moise mwaka 2021 akiwa na lengo la kuchukua nafasi hiyo ya urais.

Kuuawa kwa Moise kumeifanya Haiti, nchi iliyoko Amerika ya Kaskazini, kutokuwa na Rais kwa miaka mitano sasa.

Kukosekana kwa kiongozi kumelifanya Taifa hilo kuandamwa na magenge ya uhalifu kwa kipindi chote hicho.

Kwa sasa, Haiti iko kwenye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais unaotarajiwa kufanyika mwaka 2027.

Mapema wiki hii, mke wa Moise, Martine, ambaye alijeruhiwa katika shambulizi lililomuua mumewe, alitangaza nia ya kugombea urais.

Related articles

Recent articles