Na Malisa GJ – Facebook
HATA mimi niliwaza kama ulivyowaza wewe, lakini Malawi hii haiwezekani. Labda Rais ndo afute chama sio chama kumfuta Rais. So relax.!
Kuna dhana nyingi sana zinaweza kuwa sababu za kuangushwa kwake na utawala wake, hizi ni baadhi kwa mtazamo wangu:
Mosi, ‘over expectations’ za wananchi wao. Kutokana na kuchoshwa na chama tawala, wakaamini Wapinzani hao wangekuwa suluhisho la matatizo mengi ambayo walihisi mtawala alishindwa.
Lakini ndani ya muda mfupi wamegundua hakuna uwezekano wa kutatua mambo yao, wamemchoka. Mfano mzuri ni anguko la Rais Prof. Arthur Peter Mutharika wa Malawi na kuibuka kwa Dr. Lazarus Chakwera 2020, na kisha anguko la Chakwera na kurejea Mutharika tena uchaguzi wa mwaka 2025. Jamii ikaona bora zimwi likujualo.
Pili, amezidiwa nguvu na Spika wa Bunge ambaye alikuwa PM wake akamfukuza. Yaani ameshindana na mtu anayemzidi ushawishi kwenye mifumo ya Dola, chama chao, na Mtaani kwa Wananchi.
Alimkadiria vibaya, sasa yamemtokea puani. Spika ametumia nguvu na ushawishi wake kuendesha zoezi la kumvua uanachama na automatically jamaa anapoteza Urais. Usingashae ukiona jina la Spika ndilo linapendekezwa kuchukua nafasi ya Urais huo.
Tatu, fitna za mifumo na Chama tangulizi. Yaweza kuwa jamaa alipoingia amejikuta amerithi Mfumo ambao yeye aliuangusha so kila akijaribu kufumua mambo na kurekebisha hali, wanamkwamisha kwani wao wenyewe ndio waliharibu hali wakiwa wanatumikia Chama kilichoangushwa.
Alishinda Urais kwa kiti cha kisasa, ila amekutana na Watendaji waliotumikia Serikali iliyoangushwa kwenye Uchaguzi. Hapo lazima apate shida kupiga hatua, unafeli na jamii inaanza kukuonea kichefuchefu.
Nne, udhaifu wa uwezo binafsi wa kisiasa. Inawezekana pia Rais Faye uwezo wake kiuongozi na utendaji ni mdogo hivyo amekuwa dhaifu automatically udhaifu umeshika Serikali yote ina ‘underperform’ na hivyo jamii inazidi kumchoka kila wakati.
Chama chake kimetumia udhaifu huo pamoja na vita vyao vya kisasa, kufanya justification kumuondoa.
‘Above all’, siasa za Afrika zina utamaduni wake. Fitna ndio msingi mkuu wa siasa zetu. Binafsi naamini kilichoharakisha anguko lake Rais Faye ni ugomvi wake na Waziri Mkuu wake (sasa Spika) ambaye ameonekana kuwa na nguvu zaidi mtaani na chamani.
Naamini Chama kingemstiri iwapo angeendelea kushikamana na Waziri Mkuu wake ambaye walisota wote kabla ya ushindi.
Zimwi la siasa za Afrika za kuwagombanisha Rais na Rafiki zake wa karibu waliosota naye kabla ya ushindi, ni zimwi la hatari zaidi.
Malisa GJ ni mchambuzi wa siasa na masuala ya kijamii mwenye ushawishi mkubwa mitandaoni.


