MANCHESTER, Uingereza
STRAIKA wa Galatasaray na timu ya soka ya Taifa ya Nigeria, Victor Osimhen, yuko tayari kuisikiliza ofa ya Manchester United.
Osimhen [27], ana ndoto za kukipiga Ligi Kuu ya England kabla ya kustaafu, kwa mujibu wa Gazeti la Sun.
Mkataba wake na Galatasaray utafikia ukomo Juni, 2029, na kwa sasa mshahara wake ni Pauni milioni 13 kwa mwaka.
Kwa mujibu wa chanzo kingine cha gabari, Gazeti la Daily Mirror, staa huyo wa zamani wa Napoli yuko tayari kulipwa kiasi hicho hicho akiwa Man United.
Hata hivyo, ripoti kutoka Uturuki zinaeleza kuwa Galatasaray watakuwa tayari kumwachia Osimhen endapo itatokea klabu itakayoweka mezani Pauni milioni 100.
Man United ilitumia mkwanja mrefu kuwasajili Benjamin Sesko na Joshua Zirkzee ili kumaliza ubutu wa safu yake ya ushambuliaji, lakini nyota hao wote wameshindwa kufanya vizuri.
Takwimu zinaonesha wazi hilo kwani wawili hao wameipatia Man United jumla ya mabao manne pekee tangu msimu huu uanze.


