14.5 C
New York

Uturuki kumwachia mbunge aliyehukumiwa kifungo cha miaka 18?

Published:

STRASBOURG, Ufaransa

MAHAKAMA ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) imeiamuru Serikali ya Uturuki kumwachia huru mwanasheria ambaye pia ni mbunge, Can Atalay.

Katika taarifa yake ya leo Novemba 17, 2026, ECHR imesema Atalay anapaswa kutolewa mahabusu na kuendelea na shughuli zake za bunge.

Atalay amekuwa mtetezi wa haki za binadamu akishiriki kusimamia kesi nyingi dhidi ya waandishi wa habari na wanaharakati wanaoingia matatani kwa kuikosoa Serikali ya Uturuki.

Mwaka 203, alikuwa sehemu ya walioongoza maandamano makubwa ya vijana wa ‘Gen Z’, ambayo mamlaka zimeyahusisha na jaribio la kuipindua Serikali.

Kutokana na ushiriki wake kwenye maandamano hayo, Atalay na wenzake saba walikamatwa, wakafunguliwa mashitaka ya kujaribu kupindua Serikali, hivyo kuhukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani.

Akiwa katika Gereza la Silivri, Atalay aligombea na kushinda ubunge kupitia Chama cha Wafanyakazi cha Uturuki [TIP] katika Uchaguzi wa mwaka 2023.

Sambamba na ECHR kutaka aachiwe, pia Mahakama hiyo imeitaka Uturuki kumlipa mwanasiasa huyo fidia ya Dola za Marekani 35,700.

Related articles

Recent articles