13.1 C
New York

Klopp: Fifa ya Infantino ‘imeoza’ kuliko ya Blatter

Published:

MUNICH, Ujerumani

JURGEN Klopp amesema alidhani majanga yamekwisha ndani ya Shirikisho la Soka la Kimataifa [FIFA] baada ya Sepp Blatter kuondoshwa madarakani, kumbe hali imekuwa mbaya zaidi.

Klopp amesema FIFA ya sasa imeoza kuliko ile ya Blatter aliyeondoshwa kwa shutuma za rushwa, akisisitiza kuwa Gianni Infantino naye hapaswi kuachwa kuendelea kuliongoza Shirikisho hilo.

Blatter alilazimika kujiuzulu katika nafasi ya urasi wa FIFA mwaka 2015 kutokana na upigaji uliofichuliwa dhidi yake, hivyo Infantino kuingia madarakani Februari, 2016.

Hata hivyo, Infantino amejikuta kwenye wakati mgumu tangu alipofeli katika jaribio lake la kuuza hisa za michuano ya FIFA kwa wawekezaji binafsi.

Tangu hapo, zimekuwapo kampeni za kumtaka kujiuzulu, licha ya kiongozi huyo kuonesha nia ya kugombea tena kiti cha urais katika Uchaguzi ujao wa Machi, 2027.

“Sikufikiria kama mambo yangekuwa mabaya zaidi hata baada ya Sepp Blatter, lakini kuna mtu ameweza kufanya hivyo,” amesema Klopp.

Related articles

Recent articles