14.5 C
New York

Ndege ya jeshi Urusi yaanguka, hakuna aliyepona

Published:

MOSCOW, Urusi

NDEGE ya kijeshi ya Urusi imeanguka mjini Siberia, ambapo watu wote 19 waliokuwamo wameripotiwa kupoteza maisha.

Taarifa hiyo imetangazwa na chombo cha habari cha umma, pia ikithibitishwa na Wizara ya Ulinzi, ikieleza kuwa ndege hiyo ni aina ya An-12.

Kwa mujibu wa Wizara hiyo, chanzo cha ndege hiyo kuanguka jana Novemba 17, 2026 ni tatizo la kiufundi, ingawa uchunguzi zaidi unaendelea.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, ndege hiyo inaonekana ikianguka, pia ikiwa na viashiria vya kuwaka moto.

Hata hivyo, Gavana Ilya Seredyuk amesema timu ya uokoaji ilikimbilia eneo la tukio na kuwahi kuzima moto baada ya ndege hiyo kuanguka katika Kijiji cha Yagunovo.

Related articles

Recent articles