Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR
MECHI dhidi ya Nigeria ‘Super Eagles’ iliyochezwa leo Novemba 17, 2026, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ni ya 11 kwa kocha Miguel Gamondi tangu alipoanza kuinoa Taifa Stars.
Hata hivyo, takwimu za mechi hizo zinamuweka pabaya Muargentina huyo aliyewahi kuipa mafanikio makubwa klabu kongwe ya Yanga.
Katika mechi 11 alizokaa kwenye benchi la ufundi la Stars, Gamondi ameshinda moja pekee, sawa na wastani wa asilimia 9.1%, akifungwa sita na kutoa sare nne.
Kwamba mechi pekee aliyoshinda kocha huyo tangu alipopewa mikoba Novemba, 2025, ni ile Stars ilipoifunga Macao katika mchezo wa kirafiki wa Machi, 2026.
Aidha, mechi zake 11 kwenye benchi zimeishuhudia Stars ikifunga mabao 14, huku nyavu ikiruhusdu nyavu kutikiswa mara 16.
Michezo aliyopoteza ni dhidi ya Kuwait [4-3], Nigeria [2-1 na 3-1], Morocco [1-0], Liechtenstein [1–0], na Guinea-Bissau [2-0].
Kwa upande mwingine, michezo aliyoondoka na sare ni dhidi ya Nigeria [0-0], Madagascar [1-1], Tunisia [1-1] na Uganda [1-1].
Ni kutokana na takwimu hizo zisizoridhisha, kuna shaka kubwa juu ya nafasi ya Stars kufanya vizuri katika fainali zijazo za Mataifa ya Afrika [AFCON 2027], ambazo Tanzania itaziandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.


