14.5 C
New York

Uteuzi: Jaji Warioba ampisha Dk. Mpango

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 17, 2018, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Philip Isdor Mpango.

Dk. Mpango ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo [SUA] akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba.

Wakati huo huo, Rais Dk. Samia amemteua Bw. Ezekiel Mathias Goboro kuwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania [TAWA].

Pia, amemteua Bi. Talha Mohamed Waziri, ambaye ni Msaidizi wake, Diplomasia, kuwa balozi, kama ilivyo kwa Bw. Lucas Aaron Mayanga na Dk. Miraj Ukuti Ussi.

Related articles

Recent articles