LONDON, Uingereza
STAA wa vichekesho na filamu nchini Uingereza, Russell Brand, ameangukiwa na hukumu ya kifungo cha miaka 10 na miezi sita gerezani kwa makosa ya kubaka na kupiga wanawake.
Russell amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka manne kati ya saba yaliyokuwa yakimkabili.
Mbele ya mahakama, mwigizaji huyo ametajwa kuwa ni kiumbe katili dhidi ya wanawake na anayestahili adhabu hiyo.
Mmoja ya wanawake waliowahi kubakwa na Brand mwaka 2009 aliiambia mahakama kuwa amekuwa akiishi kwenye mateso makali ya msongo wa mawazo kila anapokumbuka aliambukizwa Ukimwi na msanii huyo.
Mahakama imejiridhisha kuwa Russels alifanya matukio hayo kati ya mwaka 2004 na 2009, yakihusisha wanawake wanne tofauti.


