MADRID, Hispania
STAA wa mchezo wa tenesi, Rafael Nadal, anatarajiwa kuwa sehemu ya Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Real Madrid.
Nadal [40[, alistaafu tenesi mwaka 2024 akiwa mshindi wa mataji makubwa 22, pia akiiwezesha timu ya taifa ya tenesi ya Hispania kutwaa mataji Matano ya michuno ya Davis Cup.
Katika kikao kitakachofanyika baadaye mwezi huu, wanachama wa Madrid watapiga kura ya kumpitisha Nadal kuwa sehemu ya wakurugenzi wao.
Nyota huyo ambaye si tu shabiki wa Madrid tangu akiwa mdogo, bali pia ni mwanachama wa klabu hiyo akiwa na kadi namba 67,778.
“Nataka kumshukuru Rais Florentino Perez na bodi kwa kunipendekeza kujiunga na bodi ya wakurugenzi ya Real Madrid,” amesema Nadal kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.


