19.8 C
New York

Waasi wavamia soko, wamuua mchungaji

Published:

BENUE, Nigeria

WATU wanne, akiwamo mchungaji, wameuawa na watu wenye silaha waliovamia soko katika Jimbo la Benue.

Tukio hilo lilitokea saa 11 jioni Jumanne ya wiki hii na mmoja ya viongozi wa eneo hilo ameeleza kuwa waasi hao walidumu kwa takribani saa mbili.

Kwa mujibu wa taarifa, waliobainika kupoteza maisha katika tukio hilo ni Msoo Chan, Pastor Terungwa Tyonungo, Suurshater Iornumbe na Dodo Shingir.

Aidha, tukio hilo limewaacha watu wengine nane wakiwa na majeraha, wakitajwa kwa majina kuwa ni Kumater Awua, Miracle Gangera, Tsetim Terungwa, Iortyom Helen, Seember Aondongu, Kofi Aondosoo, Chuku Okoro na Orker Iortyom.

Majeruhi hao wanaendelea na matibabu katika hospitali, kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo, ambaye hata hivyo aligoma kutaja jina lake kwa sababu za kiusalama.

Related articles

Recent articles