19.8 C
New York

Mtoto wa Mugabe akamatwa na polisi

Published:

HARARE, Zimbabwe

BELLARMINE Mugabe ambaye ni mtoto wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika katika shambulio.

Polisi nchini Zimbabwe wameeleza kuwa Bellarmine ni miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa kesi hiyo.

Katika shambulio hilo, kijana huyo na wengine wanne waliweza kuchukua magari mawili, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya New Zimbabwe.

Wengine waliotajwa kukamatwa wakihuishwa na tukio hilo ni Munashe Mubawu [43], Terrence Johannes Chinyemba [42], Fredson Peter [33] na Solomon Pamire [34], wakitarajiwa kupandishwa kizimbani Novemba 5, 2026.

Bellarmine mwenye umri wa miaka 29, ni mtoto wa kiume wa mwisho wa Mugabe na mkewe wa pili, Grace Mugabe.

Mugabe alifariki mwaka 2019 akiwa na historia kubwa ya kuiongoza Zimbabwe kwa miaka 37, kabla ya kuondoshwa kwa nguvu madarakani akiwa na umri wa miaka 93 mwaka 2017.

Related articles

Recent articles