19.8 C
New York

Rais Trump: Sihofii kung’olewa madarakani

Published:

WASHNGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema hahofii uwezekano wa kung’olewa madarakani na Chama cha Democrats ambacho kimeshinda Uchaguzi uliofanyika.

Democrat wameripotiwa kushinda, hivyo kwa sasa Republican cha Rais Trump kimepoteza nguvu ya kutawala Bunge na Senate.

Hiyo inawapa Democrat mamlaka ya kuongoza mihimili hiyo na wana nguvu ya kumng’oa madarakani kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais.

Hata hivyo, Rais Trump amesema hilo halimpi wasiwasi kwani anajiona ni Rais mwenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Marekani.

Katika hatua nyingine, Rais huyo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa hatua yoyote ya kumtoa Ikulu itakiangamiza Chama cha Democrat.

“Kunitoa madarakani bila sababu … Kwanini? Kwa kuwa na taifa lililofanikiwa zaidi katika historia? Nchi yetu ina mafanikio makubwa kuliko wakati wowote katika historia,” amesema Rais Trump.

Related articles

Recent articles