10.7 C
New York

Simba yaendelea kubonda, yatinga makundi CAF

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

USHINDI wa mabao 3-0 dhidi ya 15 de Agosto umeipeleka Simba katika hatua ya makundi msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, michuano ya Shirikisho la Soka barani humu [CAF].

Katika mchezo huo uliochezwa jijini Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi walipata mabao hayo ya kipindi cha pili kupitia kwa Anicet Oura (Dk. 57), Elie Mpanzu (Dk. 69) na Matlala Makgalwa (Dk. 78).

Mabao hayo yamehitimisha ushindi wa jumla ya mabao 9-1 baada ya kuifunga timu hiyo Guinea ya Ikweta mabao 6-1 kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya awali.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Guinea ya Ikweta, Simba ilishinda kwa mabao ya Ibrahim Doumbia aliyefunga mawili, Nathaniel Chilambo, Mpanzu, Makgalwa na Oura.

Baada ya mchezo huo, sasa Simba inasubiri kujua wapinzani wake wa hatua ya makundi itakayoanza kuchezwa Novemba, 2026.

Related articles

Recent articles