10.6 C
New York

Alvarez awaomba msamaha mashabiki Atletico

Published:

MADRID, Hispania

STRAIKA wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kwa kauli aliyowahi kuitoa juu ya mustakabali wake.

Wakati wa dirisha kubwa la usajili lililopita, mshambuliaji wa kati huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba anataka kuondoka klabuni hapo.

Wakati huo, staa huyo wa zamani wa Manchester City alikuwa akiwaniwa kwa karibu na Arsenal na Barcelona.

Katika kile kilichowachefua mashabiki, Alvarez alienda mbali zaidi na kusema ni ndoto yake kubwa kucheza Barcelona.

Kauli yake hiyo iliwakera mashabiki wa Atletico na tangu hapo Alvarez amejikuta akizomewa kila anapokuwa sehemu ya kikosi hicho.

“Nataka kuomba radhi kwa mashabiki wetu kwa kauli yangu wakati wa fainali za Kombe la Dunia. Lilikuwa kosa kubwa. Kwa namna nilivyosema na wakati wenyewe, haikuwa sahihi,” amesema.

Related articles

Recent articles