9.4 C
New York

Madrid wapigwa ‘stop’ kwa Vitinha

Published:

PARIS, Ufaransa

REAL Madrid haitofanikiwa katika mpango wake wa kuinasa saini ya kiungo wa PSG, Vitinha, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, amekuwa kwenye rada za mabosi wa Madrid kwa muda mrefu. Klabu hiyo inahaha kuziba mapengo ya Toni Kroos na Luka Modric.

Kwa mujibu wa wakala wake, Jorge Mendes, hakuna ofa yoyote waliyowasilisha Madrid na mchezaji huyo anafurahia kuendelea kuitumikia PSG.

Wakati huo huo, taarifa kutoka jijini Paris zinaeleza kuwa uongozi wa PSG hauna wazo la kumuuza mchezaji yeyote muhimu kikosini, akiwamo Vitinha.

Madrid walikuwa na matumaini ya kumsajili baada ya kile alichokieleza Mendes miezi michache iliyopita, aliposema mchezaji huyo anapatikana kwa klabu yoyote itakayomuhitaji.

Related articles

Recent articles