9.8 C
New York

Polisi wadaka waandamanaji 1,000 huko Ufaransa

Published:

PARIS, Ufaransa

POLISI wa Ufaransa wanawashikilia watu takribani 1,000 waliokuwa sehemu ya maandamano yaliyotikisa maeneo mbalimbali nchini humo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kutawanya waandamanaji waliokuwa wakipaza sauti kupinga ugumu wa maisha.

Maandamano hayo yaliyodumu kwa siku kadhaa za hivi karibuni yalishuhudiwa katika miji mbalimbali, ikiwamo Paris na Bordeaux.

Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani, watu zaidi ya 410,000 waliingia mitaani jana Oktoba 24, 2026.

Aidha, taarifa ya Wizara imeeleza kuwa polisi takribani 70,000 walitumika kudhibiti maandamano katika maeneo hayo.

Related articles

Recent articles