RIO, Brazil
WANANCHI wa Brazil leo Oktoba 25, 2026, wameingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa marudio wa kusaka mshindi wa kiti cha urais, huku vita ikiwa kali kati ya Luiz Inacio Lula da Silva na Flavio Bolsonaro.
Wawili hao wanarudiana baada ya Bolsonaro anayeungwa mkono na Rais wa Marekani, Donald Trump, kuongoza katika awamu ya kwanza ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 4, 2026.
Lula da Silva mwenye umri wa miaka 80 ni mwanasiasa wa mrengo wa kushoto ambaye anawania muhula wa nne [siyo mfululizo] wa kuiongoza Brazil.
Safari hii, anapata ushindani mkali kutoka kwa Seneta Flavio Bolsonaro [45], ambaye ni mwanasiasa wa mrengo wa kulia.
Bolsonaro ni mtoto wa Rais wa zamani, Jair Bolsonaro. Kiongozi huyo kwa sasa anasota gerezani baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 27 gerezani.
Hukumu hiyo ilikuja baada ya kufunguliwa mashitaka ya kusuka mpango wa kupindua Serikali baada ya kupoteza kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.


