18.1 C
New York

Ukraine imeishika pabaya Urusi

Published:

KYIV, Ukraine

ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi wa Ukraine, Oleksandr Syrskyi, amedai kuwa kwa sasa maadui zao, Urusi, wameishiwa pumzi kwenye uwanja wa vita.

Jenerali Syrskyi ameeleza kuwa Ukraine imejiimarisha zaidi kwa kuwaua wanajeshi wengi wa Urusi.

Kiongozi huyo wa zamani wa jeshi amesema hayo katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipoachia ngazi kwenye nafasi hiyo.

Alitumia mahojiano hayo kusema alifukuzwa kazi kutokana na ukosolewaji kutoka kwa wapinzani wake walioamini amekwisha kwenye mbinu za kivita.

Wakati huo huo, Syrskyi amedai kuwa Urusi imekuwa ikificha idadi sahihi ya wanajeshi wake waliouawa na Ukraine.

“Kama utahesabu waliofariki tu, idadi inaweza kuwa ni mara sita au zaidi,” amesema Styrskyi na kukanusha kashfa kubwa iliyosababisha kufukuzwa kazi.

Katika mahojiano yao na BBC, baadhi ya wanajeshi wa Ukraine waliokuwa chini ya Syrskyi walisema kiongozi huyo alikuwa akiwazuia kusonga mbele ili waingie kwenye mtego wa maadui.

Related articles

Recent articles